WENYEVITI wa serikali za mitaa na wajumbe wao katika Halmashauri ya
manispaa ya Kigoma Ujiji wameapishwa jana kuanza kutumikia wananchi
kulingana na nafasi zao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, walitaka serikali kuangalia suala la kulipa mishahara kila mwezi kwa wenyeviti na wajumbe hao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mnazi Mmoja, kata ya Kitongoni Manispaa ya
Kigoma Ujiji, Nuru Bashange alisema nafasi ya wenyeviti wa mitaa na
wajumbe wao itambulike rasmi kikatiba na walipwe mishahara kama
wanavyolipwa wabunge na madiwani.
Bashange alisema wenyeviti wa maitaa na wajumbe wao wamekuwa na
jukumu kubwa la kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo
katika maeneo yao.
Alisema imefika wakati sasa wa serikali wa kuona umuhimu wa kuwapatia
mafao ya kutosha kila mwezi viongozi hao badala ya posho ya Sh elfu
kumi kwa mwezi inayolipwa sasa.
Mwenyekiti huyo wa Mtaa alisema hata kama madiwani hawalipwi
mishahara lakini kiwango cha posho wanacholipwa hakina uwiano na kiwango
wanacholipwa wenyeviti wa mitaa.
Kwa mujibu wake, ni wakati wa kufanya maboresho kwenye malipo kuwatia
moyo wenyeviti hao katika kusimamia utendaji na utekelezaji wa mipango
ya maendeleo bila kufuata vishawishi.
Pamoja na madai hayo kwa serikali wenyeviti hao wameahidi kutumia
nafasi zao katika kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo kama ambavyo
nia na dhamira yao iliwatumia na kuamua kugombea nafasi hizo.
0 comments:
Post a Comment