Mbunge wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mohamed Raza akionesha baadhi ya vifungu
vya sheria vilivyopo kwenye kitabu kidogo cha sheria za Zanzibar,Mbele
ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo katika ukumbi wa Idara ya
Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji
wa BB Swahili nchini Tanzania,Arnold Kayanda akifanya mahojiano mafupi
na Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Raza mara baada ya
kuzungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari
MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya
waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa Mbunge wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Raza katika ukumbi wa Idara ya Habari
MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo-Globu ya Jamii
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MBUNGE wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mohamed Raza amesema Chama cha Mapinduzi
(CCM) kinaweza kutafuta mgombea wa nafasi ya urais mwenye sifa na sio
watu wanaotoa fedha kwa ajili ya kutaka kupendekezwa katika kiti hicho.
Raza
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari
MAELEZO, katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo amesema fedha
nyingi zinamwagwa Zanzibar kwa ajili ya watu wanaotaka Urais na fedha
hizo zinatoka kwa wafanyabiashara ambao watataka zirudi au kumwamulia
Rais katika nafasi za uteuzi wa baraza la mawaziri ambao watanufaika
katika kuhakikisha mambo yao yanakwenda.
Amesema
vyombo vya dola visaidie katika kupata rais mwenye sifa kwani ndiye
Amiri Jeshi Mkuu wa Ulinzi na Usalama, na bila kufanya hivyo watakaoumia
ni watanzania huku viongozi wakijinufaisha wenyewe.
Raza
amesema kuwa CCM ikifanya vibaya katika kuchagua mtu sahihi, kuna upande
wa pili wa UKAWA wana nguvu kutokana na mambo yanayoendelea nchini
kutokwenda sawa na wanatumia hoja na hawawezi kuzuilika hata wamwagiwe
maji ya pili pili wakitaka kufanya maandamano.
Raza
ambaye ni Mbunge Muwakilishi wa Jimbo la Uzini amesema kuwa hali
inayokwenda sasa sio nzuri kutokana na bajeti ya Zanzibar kukosa
wafadhili kutokana na watu waliojipatia fedha katika Akaunti ya Tegeta
Escrow wakati wazanzibar hawajahusika kujipatia fedha hizo.
Amesema
kutokana na kukwama kwa wafadhili, wanaoathirika ni wananchi kwani posho
ya mbunge ya siku ndio fedha ya mwananchi ya mwezi mmoja hivyo kutokana
na dola kushuka wataathirika kwa kiwango kikubwa.
"Aidha
kutokana mambo yanayoendelea tunahitaji kuwa na viongozi ambao
wanaangalia wananchi na sio wale ambao wanajiangalia wenyewe kwa
masilahi yao binafsi huku wanaowagua wakiwa na hali mbaya",alisema
Raza.(Muro)
0 comments:
Post a Comment