Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ameendelea kumwaga misaada kwa wadau na
makundi mbalimbali ya wananchi katika jimbo lake, Pichani, Mtemvu
akizungumza kabla ya kuanza kugawa zawadi hizo kwa ambao hawakuzipata
wakati wa Mfungo uliopita wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, zaidi ya
wananchi 900 walipata zawadi hizo alizogawa jana kwenye viwanja vya
Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.
Mtemvu akionyesha chupa ya chai ambayo ni miongoni mwa seti za vifaa vya nyumbani alivyozawadia wananchi katika hafla hiyo.
Mtemvu akimkabidhi mgawo wake, Tatu Ligalwike
Mtemvu akimkabishi zawadi yake, Mohammed Mbonde, ambaye sasa ni Mjumbe
wa Baraza la wazee wa CCM Temeke, ambaye amewahi kuwa Katibu wa CCM
katika mikoa mbalimbali ukiwemo wa Shinyanga.
Wadau kabla ya kukabidhiwa zawadi hizo
Wadau wakiwa wamekaa kwenye madawati mapya kabla ya kupewa zawadi hizo,
Katika hafla hiyo Mtemvu alikabidhi pia madawati 100 kwa viongozi wa
Kata mbili ikiwemo ya sandali
Mtemvu akikabidhi madawati 50 kwa Diwani wa Kata ya Sandali Abel Tarimo.
Jumla 13, zimeshanufaika na msaada wa mawati wa Mbunge huyo.
0 comments:
Post a Comment