Kufuatia
kuripotiwa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na
mgogoro wa mpaka uliokuwepo kutokana na madai kuwa kisiwa cha Pemba ni
sehemu ya Kenya, Serikali ya Tanzania imetoa taarifa rasmi kuhusiana na
mgogoro huo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe, amewatoa hofu
Wananchi kuwa Pemba ni sehemu ya Tanzania na hakuna ukweli wowote
kwamba kisiwa hicho ni sehemu ya Kenya.
Akijibu kuhusiana na suala hilo jana Bungeni Dodoma Membe alisema;
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijapata taarifa zozote
rasmi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Kenya kuhusu mgogoro wa mpaka kati
ya Serikali hizi mbili… hususan madai ya kisiwa cha Pemba kilicho ndani
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni sehemu ya Jamhuri ya Kenya..
Kisiwa cha Pemba ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
kitaendelea kubakia hivyo daima…
“Wizara yangu iliwasiliana na ubalozi wetu Kenya lakini pia tuliwasiliana na Serikali ya Kenya yenyewe.. kucheki kama taarifa hizi zilizoandikwa kwenye magazeti zina mshiko wa Serikali, balozi wetu na serikali yenyewe ya Kenya hawajui suala hili limetokea wapi”
Kuhusiana na taarifa za kuwepo meli za kutoka Kenya zinazofanya shughuli za uvuvi katika eneo la Tanzania, Membe alisema; “Nitawasiliana
na wenzangu wanaohusika.. kuanzia wizara inayohusika na JWTZ ambao ndio
wana dhamana ya kulinda bahari yetu ya Indian Ocean waone namna ya
kudhibiti na namna ya kuwahakikishia wenzetu wa Kenya kwamba hata
baharini kuna mipaka yake”
0 comments:
Post a Comment