WAKATI siku zikishika kasi kuelekea uchaguzi mkuu mwakani,’Bundi’ ametua ndani ya CHADEMA mkoa wa Singida na hali imechafuka kwa viongizi wake kuanza kuvuana uanachama na kufukuzana uongozi.
Baraza la uongozi mkoa wa Singida, limemvua na kumfukuza uongozi Mwenyekiti wa jimbo la Singida mjini,John Kalaye Kumalija kwa tuhuma ya kuwa na mgogoro wa muda mrefu na katibu wake.
Uamuzi huo umeaanza kutekelezwa kuanzia Oktoba saba mwaka huu.
Hayo
yamo kwenye barua iliyoandikwa na Katibu baraza la uongozi mkoa wa
Singida,Patrick Mssuta ya Oktoba saba mwaka huu, isiyokuwa na
kumbukumbu.
Aidha,kwa
mujibu wa baraua hiyo, inadai Mwenyekiti huyo alifanya kitendo cha
utovu wa nidhamu kwa kugombana hadharani na Katibu wake Yahaya Ramadhan.
Kutokana na uamuzi huo,baraza la uongozi mkoa wa Singida limemwagiza Kumalija kukabidhi ofisi mara moja kwa katibu mwenezi wa jimbo,mwenyekiti wa baraza la wazee au kamati ya utendaji ya jimbo.
“Pia unatakiwa kutojishughulisha na shughuli za uongozi au za chama kwa muda huu ukiwa chini ya uangalizi maalum wa chama”, imesema barua hiyo.
Hata hivyo,Katibu Mssuta katika barua yake hiyo, amejichanganya baada ya kichwa cha habari kusomeka kuwa Kumalija anasimamishwa uongozi, halafu ndani ya maelezo yake amesema baraza la uongozi mkoa,limemvua na kumfukuza uongozi.
Kwa upande wake Kumalija amejibu mapigo kwa barua yake ya Oktoba 31 mwaka huu ambayo nayo haina kumbukumbu.
Katika barua yake,Kumalija amedai kuwa hana mgogoro wowote na katibu wake Yahaya Ramadhan.
“Baraza lako halina mamlaka yoyote ya kunisimamisha na kunivua uongozi.Mamlaka ya kuchukua/kutoa maamuzi hayo ni mkutano mkuu wa wilaya au jimbo,” Kumalija amesema na kuongeza;
“Kwa
sababu hizo na zingine,Mimi John Kalaye Kumalija,najitambua kuwa bado
ni mwenyekiti halali wa CHADEMA jimbo la Singida mjini”.
0 comments:
Post a Comment