Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua jambo mbele ya waandishi
wa Habari leo (hawapo pichani) ,jijini Dar es Salaam, kuhusiana na
kubadilika kwa tarehe ya mkutano wao kufuatia kuingiliana na Mkutano wa
Baraza la Wawakilishi.
Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye Akizungumza na waandishi wa Habari
leo ,jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kubadilika kwa tarehe ya mkutano
wao kufuatia kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
Na Chaalila Kibuda,Globu ya Jamii.
KAMATI
kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inatarajia kukutana Mei 23 mjini Dodoma
na kujadili ajenda mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu .
Akizungumza
na waandishi wa Habari leo ,jijini Dar es Salaam,Katibu wa Halmashauri
Kuu Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kuwa kubadilika kwa siku ya
mkutano imetokana na kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
Nape
amesema kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kitafanyika Mei 22 ambapo ajenda
mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na maoni ya Ilani ya CCM
2015-2020 ambayo itawasilishwa na Kamati iliyoundwa kwa kazi hiyo.
Amesema
kutakuwa na vikao vya kawaida Mei 21 hadi 22 ambavyo vitakuwa
vinafanyika mkoani Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya
Mkutano wa Kamati kuu ya CC na Halmashauri Kuu (NEC).
Nape
amesema vikao hivyo vitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete
katika kujadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya siasa ya chama
hicho.
Wakati
huo huo Nape amesema kuwa wanachama sita waliofungiwa bado hatma yake
kutokana na suala hilo linashughulikiwa na kamati mbili ambazo ndizo
zinaweza kusema kifungo kinaendelea ama la,amesema na kuongeza kuwa
Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaongozwa na kanuni ambazo yeye mwenyewe
amezikuta hivyo ni lazima wanachama na makada wazifuate kanuni na
miongozo ya chama.
Amesema
wanachama kutangaza nia ya kugombea sio tatizo lakini mazingira
yanayoendana baada ya kutangaza nia hiyo ndipo kanuni na miongozo ya
chama inaanza kutumika,amesema kanuni na miongozo ya CCM zinasema mtu
ambaye yuko kwenye kifungo katika chama haruhusiwi kugombea nafasi
yeyote ndani ya chama ambazo zipo wazi.
Amesema
mikutano hiyo itajadili jinsi gani watu watapochukua fomu,urudishaji wa
fomu pamoja na njia ambazo zitatumika katika utangazaji nia kwa wagombea
kutokana na mazingira yaliyopo.
0 comments:
Post a Comment