728x90 AdSpace

Latest News

Wednesday, October 1, 2014

KINANA ASAFIRI NA WANANCHI KWA BAISKELI AKITOKA LUSHOTO KWENDA MKINGA, TANGA

 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakisafiri kwa baiskeli wakati walipokuwa wanatoka wilayani Bumbuli kwenda wilaya ya Mkinga, leo Septemba 30, 2014, Kinana akiwa katika ziara ya kukagua na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Tanga.
 Safari ya Kinana na Nape kwa baiskeli ikiendeleza kukatiza milima na mabonde kutoka wilaya ya Lushoto kwenda Mkinda
 Kinana akiongoza msafara wa safari hiyo kwa baiskeli kutoka Lushoto kwenda Mkinga
 Nape akiwasili kwa baiskeli katika Kijiji cha  Mng'aro, wilayani Lushoto mkoa wa  Tanga
Kinana na Nape wakifuahi baada ya kuwasili salama katika Kijiji cha Mng'aro kwa safari ya baikeli
Wanahabari waliosafiri kwa baiskeli wakipumzika baada ya kufika katika Kata ya Mng'aro

 Wananchi wa Kijiji cha Mng'aro wakimlaki Kinana baada ya kuwasili katika Kijiji hicho kwa baiskeli
 Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mng'aro waliompokea alipowasili kwenye kijiji hicho kwa baiskeli, leo Septemba 30, 2014 akienda wilaya ya Mkinga
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimia wananchi wa Kijiji cha Mng'aro alipowasili na Kinana kwa baiskeli katika Kijiji hicho
 Mkuu wa wilaya ya Lushoto, Majid Mmanga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mng'aro baada ya kuwasili na Kinana kwa baiskeli katika kijiji hicho
 Kinana akisalimiana na viongozi wa CCM baada ya kuwasili katika wilaya ya Mkinga
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati katika Kata ya Daluni baada ya kuwasili katika wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, leo Septemba 30, 2014
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Mkinga baada ya kushiriki ujenzi wa zahanati. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye.
 Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili Kituo cha Polisi kata ya Maramba, kushiriki ujenzi wa kituo hicho .
 Vijana wakiwa katika kazi ya kuchanganya mchanga na saruji kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha polisi
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Mkinga wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani) alipozungumza nao katika ukumbi wa World Vision, wilayani humo.
Wananchi wakishangilia huku mmoja wapo akiwa na bango la kuisifia CCM katika mkutano huo wa hadhara.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Maforoni,  Kata ya Duga.
Kinana akizawadiwa mswala uliotolewa na wanakijiji
Kinana akihutubia katika mkutano huo wa hadhara katika Uwanja wa Maforoni, Duga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: KINANA ASAFIRI NA WANANCHI KWA BAISKELI AKITOKA LUSHOTO KWENDA MKINGA, TANGA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top