Mhe. Mjenga akifanya mazungumzo kati Mwenyekiti Lootah, katika ofisi za Nakheel.
Mhe. Omar Mjenga akutana na Mwenyekiti
wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai (NAKHEEL) Bwa. Rashid Lootah.
Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai, mhe.
Omar Mjenga, leo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Bw. Rashid Lootah,
Mwenyekiti wa Nakheel, Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai.
Katika mazungumzo yao, wamezungumzia
ziara ya Mwenyekiti huyo pamoja na ujumbe wake kuitembelea Tanzania,
itakayofanyika kuanzi tarehe 16-20 Septemba, ambako anatarajia pamoja na
kuonana na baadhi viongozi wa Serikali, watafanya mazungumzo na Shirika la
Nyumba la Taifa(NHC) yatakayowezesha kusainiwa makubaliano ya ushirikiano kwenye
sekta ya nyumba kati ya mashirika hayo mawili.
Aidha, watapata fursa ya kukitembelea
kituo cha uwekezaji - TIC ili kupata taarifa muhimu za uwekezaji.
Aidha, Mhe. Mjenga amemuomba Mwenyekiti
huyo kufadhili mkutano wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Utalii utakaofanyika
Novemba hapa Dubai. Mkutano huo unaandaliwa na Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana
na Bodi ya Utalii ya Tanzania-TTB pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.
|
0 comments:
Post a Comment