Mjumbe wa Kamati kuu
ya CCM Mhe.Jerry Silaa ambaye ni Mlezi wa mkoa wa simiyu juzi katika siku ya
sita ya ziara yake amekagua utekelezaji wa ahadi ya Mhe Rais Dr.Jakaya Kikwete ya
ujenzi wa barabara za lami kilometa 3 kwenye mji wa Mwanhuzi makao makuu
ya Wilaya ya Meatu.
Kazi imefanyika kwa 40% na itakamilika mwezi wa
tatu mwakani.
Mojawapo ya mitambo ya
kutengeneza barabara hiyo ikiwa kazini,Mhe Silaa anaendelea na ziara
yake ya siku kumi mkoani simiyu ambapo leo ameingia katika siku ya sita
katika mkoa huo ambao yeye ndiye mlezi wa CCM mkoa huo.
0 comments:
Post a Comment