Ujumbe wa Zanzibar uliokuwa nchini China kwa ziara ya Kiserikali
ukipata mlo kwenye Tafrija maalum waliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania
Nchini China.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. Said
Hassan Said, Meya wa Manispaa ya Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman
Khatib, Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla
Shaaban,Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali
Mbarouk na Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Mh. Ussi Jecha Simai.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi
akiwa pamoja na Mke wa Balozi wa Tanzania Nchini China Mama Mary Antony
Tairo pamoja na Afisa wa Ubalozi huo Nd. Kitokezi Juma Kitokezi wakiwa
kwenye Tafrija iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Nchini China kwa
ujumbe wa Zanzibar.
Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya China { BCEG }
Mhandisi Tiger Nzu akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wake ulipofanya ziara ya kutembelea
uwanja wa Kimataifa wa Beijing Nchini China ambao umejengwa na Kampuni
hiyo ya BCEG.
Nyuma ya Mhandisi Tiger Nzu ni Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na
Michezo Mh. Said Ali Mbarouk, kati kati ya Balozi Seif na Mh. Said ni
Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo,
kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh.
Ramadhan Abdulla Shaaban na nyhuma yake ni Mwakilishi wa Jimbo la Chaani
Mh. Ussi Jecha Simai.
Balozi
Seif akizungumza mara baada ya Tafrija iliyoandaliwa na Kampuni ya
Ujenzi ya BCEG kwa ajili ya Ujumbe wake baada ya kumaliza kutembelea
uwanja wa ndege wa Beijing Nchini China.
Mbele ya Balozi Seif aliyevaa miwani na kukaa ni Naibu Meneja wa Kampuni ya BCEG Bwana Dinng Chuanbo.
0 comments:
Post a Comment