SHIDAAA:MGOMBEA UENYEKITI CHADEMA AWAKIMBIA VIONGOZI CHADEMA: KUKWEPA KUTOA UFAFANUZI WA PINGAMIZI ALILOWEKA DHIDI YA MBOWE:
MGOMBEA nafasi ya Uenyekiti Taifa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,
(CHADEMA), Kansa Mbarouk, amedaiwa kuwakwepa viongozi wa chama hicho
wanaotaka kumpa barua ya wito kufika kusikiliza ufafanuzi wa pingamizi
lake alilomwekea mgombea mwenzake, Freeman Mbowe.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, Mbarouk
wanamtafuta toka Septemba 8 ili achukue barua yake ya kuitwa kwenye
vikao viwili lakini hadi sasa anapiga chenga.
Makene alisema juhudi mbalimbali zimefanyika ikiwamo kupigiwa simu aeleze aliko, lakini zote zimegonga mwamba.
“Ni kama hataki…akipigiwa simu anapokea lakini akiambiwa aje kuchukua
haonekani, wala akiambiwa apelekewe anaonekana hataki,” alisema na
kuongeza.
Kwanza tumekiri kupokea barua yake ya Septemba 5 mwaka huu, ambayo
imepokelewa ofisini kwa Katibu Mkuu Septemba 8 saa 8:29 mchana.
Pia alitakiwa Septemba 10 saa 10 jioni afike makao makuu saa 10 jioni
kukutana na Kamati ya Uchambuzi wa fomu za wagombea kwa hatua za awali
za kushughulikia pingamizi lake na masuala yanayohusu ugombea wake kama
inavyoelezwa na kanuni za chama kifungu cha b 7:2:7.
“Kwa sababu hiyo, tumemfahamisha yafuatayo; (a)Kamati Kuu itakaa
Septemba 12 kwa ajili ya uteuzi wa wagombea kwa mujibu wa kanuni za
chama kifungu cha 7:2:6 (b) tumemtaarifu kuwa anatakiwa kuhudhuria kikao
hicho ambacho pamoja na mambo mengine kitajadili na kuamua juu ya
pingamizi lake,” alisema..
Taarifa zinasema kuwa Mbarouk, mmoja ya wanachama wanne wa CHADEMA
waliojitokeza kuwania kiti hicho aliitwa kufika mbele ya kikao cha
kamati ya uchujaji ya Uchaguzi wa Taifa jana saa kumi jioni lakini
hakujitokeza.
Wito huo ulidaiwa ni kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa kazi za chama kifungu cha 7.2.7.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebainikuwa Mbarouk
alishaandikiwa barua kumwarifu kuwa barua yake ilifika siku ya Jumanne,
Septemba 8, saa 8:29 mchana, ingawa siku moja kabla pingamizi hilo
lilionekana kwenye baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Pingamizi la Mbarouk lilifika Makao Makuu ya Chama hicho siku 3 tangu lilipoandikwa.
Kufikia jana jioni taarifa zilikuwa zikisema kuwa Mbarouk hapokei
simu wala kueleza mahali alipo ili aweze kupelekewa barua yake ya wito
iliyokuwa ikimtaka afike kwenye kamati.
Juhudi za kumtafuta Mbarouk kwa simu jana, ziligonga mwamba hadi tunakwenda mitamboni.
0 comments:
Post a Comment