Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisoma risala ya
kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs)
kwa wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa
wa serikali kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za shirika hilo jijini
Dar.
Na Mwandishi wetu
MRADI
wa miaka minne wa kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa
kufanikisha majaribio ya maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la elimu na sayansi na utamaduni (UNESCO) na kuendeshwa
na wizara ya elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34
umemalizika kwa mafanikio huku wito ukitolewa kutafutwa njia ya
kuendeleza mradi huo.
Tangu awali mradi huo haukuelezwa kinaga ubaga unakuaje endelevu kama utaonekana kuwa na manufaa kwa taifa.
Akitoa maelezo ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu,wataalamu na maofisa wa serikali, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania,
Bi. Zulmira Rodrigues aliwataka wadau hao kuzingatia mafanikio
yaliyokuwapo,kuangalia changamoto zake na kuona namna ya kuendeleza
mazuri ya mradi.
Mradi
huo wa majaribio ulifanyika katika shule za mikoa ya Mbeya,
Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Kagera, Morogoro, Kigoma na
Tanga kwa upande wa Tanzania Bara.
Aidha
ilielezwa katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Unesco kwa lengo
la kuufunga rasmi pamoja na malengo yake ya kuboresha elimu Tanzania kwa
kuhakikisha masomo ya sayansi yanafundishwa kwa namna inavyotakiwa,
tathmini ilionesha udhaifu wa kutokuwepo na mpango madhubuti wa
kuendelezwa kwake.
Mradi
huu wa majaribio wa MSK ulilenga kukuza uwezo wa kufundisha masomo ya
sayansi (baiolojia,kemia na fizikia) kwa shule ambazo hazina maabara
kwakuzipatia visanduku vya majaribio pia uliendesha warsha mbalimbali
ili kukuza uwezo wa matumizi ya zana zilizo katika mradi wa MSK pamoja
na vitabu vya kufundishia.
Aidha
mradi huo ulizingatia pia kuongeza upendo wa masomo ya sayansi kwa
jamii na kuwafanya wanafunzi wapende na wawe na hamu na masomo ya
sayansi.
Mradi
huo ambao umefanyika kwa kuzingatia pia mahitaji ya taifa na kimataifa
chini ya dhana ya kuendeleza masomo ya sayansi duniani unaendeshwa na
UNESCO kwa kujenga uwezo wa shule za sekondari na msingi kufanya mazoezi
ya utambuzi wa nadharia mbalimbali kimaabara hutoa masanduku maalumu
ambayo yanakuwa ni kama maabara ndogo zinazotembea.
Maabara
hizi hutoa uwezo wa kufanyika kwa majaribio ya msingi na yale makubwa
kwa kuzingatia madaraja mbalimbali ya mafunzo kuanzia ngazi za chini
kati na juu.
Katika
ufungaji wa mradi huo uliofanyika mwishoni mwa mwezi Agosti washiriki
walielezwa maendeleo ya mradi hadi mwisho wake na changamoto zilizokuwa
zinakabiliwa.
Unesco
imesema kutanuka kwa kasi kwa elimu ya msingi kumesababisha changamoto
za ubora wa elimu katika mfumo wa elimu nchini na mradi wa majaribio
ulionesha kwamba ubora unaweza kurejeshwa kwa kuwa na mpango kama MSKs.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali,
maafisa elimu na maofisa wa serikali waliohudhuria mkutano huo
uliofanyika mwishoni mwa juma.
Kutokana
na changamoto za raslimali kushindwa kuhakikisha kwamba kila darasa,
mwalimu na mwanafunzi wanakuwa na zana zinazotakiwa kufundisha na
kujifunza,walimu na wanafunzi walielemewa na hivyo kuathiri ufundishaji
wa masomo ya sayansi ya baiolojia, kemia na fizikia.
Mathalani
matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2011 wastani wa matokeo ya masomo ya
sayansi kitaifa uliporomnoka chini ya asilimia 50.
Fizikia
ilikuwa aislimia 43.2, kemia 43.3 na baiolojia 43.4 na katika takwimu
hizo zilionesha kwamba wasichana walifanya vibaya zaidi.
Utafiti
ulionesha wazi kwamba udhaifu huo umetokana na kukosekana kwa maabara,
vifaa vya kufundishia na upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi.
Pamoja
na kuwepo kwa changamoto za uhaba wa masanduku haya ya maabara,
tathmini iliyiofanywa ilionesha kwamba mradi ungeliweza kuunganishwa na
miradi kama ya JICA na pia kutengenezewa mfumoi wa wa kuweza kuwa
endelevu kutokana na umuhimu wake na ufanisi.
Changamoto
kama za masanduku machache kuliko yalivyokusudiwa katika mradi , muda
mfupi wa kufunza walimu na pia kutekeleza yote yaliyopangwa na suala la
ukaguzi bado mradi huu kutokana na asili yake ungelikuwa na maana zaidi
kuendelezwa ili kufikia zaidi shule zilizo pembezoni.
Aidha
ili kuendelea na mradi huo tathmini iliyofanywa na kuelezwa na Ellen
Binagi katika kikao cha wadau ilishauriwa serikali kufikiria kuanzisha
vituo na taasisi za kutengeneza maabara hizo ndogo nchini badala ya
kuagiza kutoka nje kutokana na gharama zake na hasa ikizingatiwa kwamba
Tanzania ni nchi kubwa na yenye shule nyingi.
Binagi
alisema kwamba kuanzishwa kwa mtindo huo kumeleta muonekano mpya katika
upenzi wa masomo ya sayansi na katika shule za majaribio ufanisi wake
ulikuwa mkubwa na ipo haja ya kuangalia namna ya kuendeleza.
Mtathmini
huyo pia amesema ipo haja kwa UNESCO na serikali ya Tanzania pamoja na
mradi kumalizika kuona namna ya kuuendeleza na kuondoa changamoto
zilizoonekana wakati wa utekelezaji wake.
0 comments:
Post a Comment