Makundi
mbalimbali ya wananchi yamekuwa yakimtakia uponaji wa haraka kwa njia
ya ujumbe mfupi wa simu.
Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume wiki iliyopita na afya yake imekuwa ikiimarika siku hadi siku.
Miongoni mwa waliomtakia afya njema ni familia
ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambayo imeeleza kupokea kwa
masikitiko taarifa za kuugua kwake na kumwombea apone haraka ili
aendelee na majukumu yake kwa Taifa.
Chama cha RPP cha
Rwanda kimemtumia salamu za pole Rais Kikwete na kuungana na mamilioni
ya Watanzania kumwombea ili arejee katika afya yake na majukumu ya kila
siku.
“RPP tutashirikiana na familia, marafiki na
mamilioni ya Watanzania kumwombea Rais Kikwete aweze kupona haraka. Rais
Kikwete ni jirani yetu na mtetezi mkubwa wa kanda hii katika kupata
ukombozi wa kijamii, kisiasa na kiuchumi,” ilisema taarifa ya RPP kwa
umma iliyotolewa na Rais wa chama hicho, John V Karuranga.
Aondoka wodini
Wakati Rais
Kikwete akiondoka wodini, alikuwa anatembea akiwa amesindikizwa na
daktari bingwa, Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins na
mkewe Salma.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais, Ikulu iliyotolewa juzi ilisema: “Afya yake imekuwa inaimarika
kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea na akiwa katika hoteli hiyo,
ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.”
Iliongeza:
“Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembelewa mara kwa mara
na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja
baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari
kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.”
Taarifa hiyo
ilisema: “Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao nao
umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete atakuwa katika hoteli maalumu
(haikutajwa), iliyo na uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins.”
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Daktari Bingwa Edward
Schaeffer kutoka
Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa
upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita.Kulia ni Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer muda
mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins huko
Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji mwishoni
mwa wiki iliyopita.(picha na Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment