728x90 AdSpace

Latest News

Tuesday, November 4, 2014

ANGALIA MAFANIKIO YA ILANI YA CCM:MANISPAA YA MOSHI KUWA JIJI IFIKAPO 2015

MKOA wa Kilimanjaro umepitisha rasmi azimio la kuiomba Serikali kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kuwa jiji ifikapo mwaka 2015.
 
Azimio hilo limepitishwa katika kikao cha ushauri cha mkoa huo (RCC), chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa, Leonidas Gama ambaye amewataka watendaji wa ngazi mbalimbali kutekeleza vigezo vichache vilivyobaki ili kupandishwa hadhi hiyo.
 
Alisema miongoni mwa vigezo vikubwa vilivyokuwa vikihitajika ni pamoja na kuongeza ukubwa wa eneo la Manispaa hiyo kutoka kilomita za mraba 58 za sasa hadi kufikia kilometa 142, jambo ambalo tayari limetekelezwa.
 
Alisema upanuzi wa manispaa hiyo unajumuisha vijiji tisa kutoka Halmashauri ya wilaya ya Moshi Vijijini na vijiji viwili kutoka Halmashauri ya wilaya ya Hai ambapo kilomita za mraba 84 zinaongezwa ili kutimia kilomita za mraba 142 zitazowezesha Moshi kuwa Jiji.
 
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Shaaban Ntarambe alikihakikishia kikao cha RCC kuwa taratibu zote muhimu zimetekelezwa, ikiwamo elimu kwa wananchi wa vijiji vitakavyoingizwa katika hadhi ya jiji na kuwaondoa hofu iliyojengwa na baadhi ya wanasiasa kuwa wanapora ardhi yao.
 
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Moshi, Japhar Michael kwa nyakati tofauti alikuwa akielezea kuwa mipango ya upanuzi wa Manispaa hiyo halitahusisha mwananchi kunyang’anywa ardhi na mashamba kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa.
 
Alisema mipango hiyo ambayo ina faida kwa wakazi wa manispaa hiyo na wengine watakaojiunga na jiji hilo, unafanyika kwa kutumia busara na elimu zaidi kwa wananchi kuliko kutumia mabavu.
 
Mpango wa Manispaa hiyo kuwa Jiji uliungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete tangu mwaka 2012 alipofanya ziara mkoani humo ambapo baada ya kuelezwa lengo hilo alitaka viongozi katika halmashauri husika kukutana ili kuondoa tofauti zinazojitokeza ili lengo litimie mwaka 2015.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: ANGALIA MAFANIKIO YA ILANI YA CCM:MANISPAA YA MOSHI KUWA JIJI IFIKAPO 2015 Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top