728x90 AdSpace

Latest News

Thursday, September 11, 2014

SHIDAAA:MGOMBEA UENYEKITI CHADEMA AWAKIMBIA VIONGOZI CHADEMA: KUKWEPA KUTOA UFAFANUZI WA PINGAMIZI ALILOWEKA DHIDI YA MBOWE:

MGOMBEA nafasi ya Uenyekiti Taifa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Kansa Mbarouk, amedaiwa kuwakwepa viongozi wa chama hicho wanaotaka kumpa barua ya wito kufika kusikiliza ufafanuzi wa pingamizi lake alilomwekea mgombea mwenzake, Freeman Mbowe.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, Mbarouk wanamtafuta toka Septemba 8 ili achukue barua yake ya kuitwa kwenye vikao viwili lakini hadi sasa anapiga chenga.

Makene alisema juhudi mbalimbali zimefanyika ikiwamo kupigiwa simu aeleze aliko, lakini zote zimegonga mwamba.

“Ni kama hataki…akipigiwa simu anapokea lakini akiambiwa aje kuchukua haonekani, wala akiambiwa apelekewe anaonekana hataki,” alisema na kuongeza.

Kwanza tumekiri kupokea barua yake ya Septemba 5 mwaka huu, ambayo imepokelewa ofisini kwa Katibu Mkuu Septemba 8 saa 8:29 mchana.

Pia alitakiwa Septemba 10 saa 10 jioni afike makao makuu saa 10 jioni kukutana na Kamati ya Uchambuzi wa fomu za wagombea kwa hatua za awali za kushughulikia pingamizi lake na masuala yanayohusu ugombea wake kama inavyoelezwa na kanuni za chama kifungu cha b 7:2:7.

“Kwa sababu hiyo, tumemfahamisha yafuatayo; (a)Kamati Kuu itakaa Septemba 12 kwa ajili ya uteuzi wa wagombea kwa mujibu wa kanuni za chama kifungu cha 7:2:6 (b) tumemtaarifu kuwa anatakiwa kuhudhuria kikao hicho ambacho pamoja na mambo mengine kitajadili na kuamua juu ya pingamizi lake,” alisema..

Taarifa zinasema kuwa Mbarouk, mmoja ya wanachama wanne wa CHADEMA waliojitokeza kuwania kiti hicho aliitwa kufika mbele ya  kikao cha kamati ya uchujaji ya Uchaguzi wa Taifa jana saa kumi jioni lakini hakujitokeza.

Wito huo ulidaiwa ni kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa kazi za chama kifungu cha 7.2.7.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebainikuwa Mbarouk alishaandikiwa barua  kumwarifu kuwa barua yake ilifika siku ya Jumanne, Septemba 8, saa 8:29 mchana, ingawa siku moja kabla pingamizi hilo lilionekana kwenye baadhi ya vyombo vya habari nchini.

Pingamizi la Mbarouk lilifika Makao Makuu ya Chama hicho siku 3 tangu lilipoandikwa.

Kufikia jana jioni taarifa zilikuwa zikisema kuwa Mbarouk hapokei simu wala kueleza mahali alipo ili aweze kupelekewa barua yake ya wito iliyokuwa ikimtaka afike kwenye kamati.

Juhudi za kumtafuta Mbarouk kwa simu jana, ziligonga mwamba hadi tunakwenda mitamboni.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: SHIDAAA:MGOMBEA UENYEKITI CHADEMA AWAKIMBIA VIONGOZI CHADEMA: KUKWEPA KUTOA UFAFANUZI WA PINGAMIZI ALILOWEKA DHIDI YA MBOWE: Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top