728x90 AdSpace

Latest News

Monday, May 18, 2015

KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA MEI 23,DODOMA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari leo (hawapo pichani) ,jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kubadilika kwa tarehe ya mkutano wao kufuatia kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye Akizungumza na waandishi wa Habari leo ,jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kubadilika kwa tarehe ya mkutano wao kufuatia kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
Na Chaalila Kibuda,Globu ya Jamii.
KAMATI kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inatarajia kukutana Mei 23 mjini Dodoma na kujadili ajenda mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu .
Akizungumza na waandishi wa Habari leo ,jijini Dar es Salaam,Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kuwa kubadilika kwa siku ya mkutano imetokana na kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
Nape amesema kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kitafanyika Mei 22 ambapo ajenda mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na maoni ya Ilani ya CCM 2015-2020 ambayo itawasilishwa na Kamati iliyoundwa kwa kazi hiyo.
Amesema kutakuwa na vikao vya kawaida Mei 21 hadi 22 ambavyo vitakuwa vinafanyika mkoani Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Kamati kuu ya CC na Halmashauri Kuu (NEC).
Nape amesema vikao hivyo vitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete katika kujadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya siasa ya chama hicho.
Wakati huo huo Nape amesema kuwa wanachama sita waliofungiwa bado hatma yake kutokana na suala hilo linashughulikiwa na kamati mbili ambazo ndizo zinaweza kusema kifungo kinaendelea ama la,amesema na kuongeza kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaongozwa na kanuni ambazo yeye mwenyewe amezikuta hivyo ni lazima wanachama na makada wazifuate kanuni na miongozo ya chama.
Amesema wanachama kutangaza nia ya kugombea sio tatizo lakini mazingira yanayoendana baada ya kutangaza nia hiyo ndipo kanuni na miongozo ya chama inaanza kutumika,amesema kanuni na miongozo ya CCM zinasema mtu ambaye yuko kwenye kifungo katika chama haruhusiwi kugombea nafasi yeyote ndani ya chama ambazo zipo wazi.
Amesema mikutano hiyo itajadili jinsi gani watu watapochukua fomu,urudishaji wa fomu pamoja na njia ambazo zitatumika katika utangazaji nia kwa wagombea kutokana na mazingira yaliyopo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA MEI 23,DODOMA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top