728x90 AdSpace

Latest News

Monday, September 15, 2014

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AMLILIA IGP ERNEST MANGU..SABABU HII HAPA

MEYA wa Ilala, Jerry Silaa amemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Ernest Mangu kutokubali askari wake kuwa wakala wa sheria za barabara.
 
Silaa alisema hayo katika uchaguzi wa Naibu Meya uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Alisema askari wengi wanajichukulia sheria mkononi kwa kuwakamata baadhi ya madereva kwa madai kuwa magari yao yamezidi viwango hivyo yanaharibu barabara pasipo kuzingatia sheria.

Pia Silaa ameitaka Mahakama ya Jiji kuacha kuwakamata wananchi kwa makosa yasiyofaa na ambayo hayana uhakika, kuwatoza faini zisizo na msingi na kuwaweka mahabusu bila hatia.

“Ninapigiwa simu na kupewa malalamiko mara kadhaa wananchi wanaonewa bila sababu za msingi na kuwafanya wajione sawa na wakimbizi katika nchi hii,” alisema Silaa.

Pamoja na hayo alisaini mkopo wa sh bilioni 1.2 kutoka Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) kwa ajili ya kununua magreda mawili ya kutengeneza miundombinu ya halmashauri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AMLILIA IGP ERNEST MANGU..SABABU HII HAPA Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top