728x90 AdSpace

Latest News

Friday, August 29, 2014

Balozi wa Tanzania Dubai..Mhe. Omar Mjenga akutana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai

Mhe. Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Lootah mbele ya baadhi ya miradi inayojengwa na Nakheel.
Mhe. Mjenga akifanya mazungumzo kati Mwenyekiti Lootah, katika ofisi za Nakheel.
Mhe. Omar Mjenga akutana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai (NAKHEEL) Bwa. Rashid Lootah.
Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai, mhe. Omar Mjenga, leo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Bw. Rashid Lootah, Mwenyekiti wa Nakheel, Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai.
Katika mazungumzo yao, wamezungumzia ziara ya Mwenyekiti huyo pamoja na ujumbe wake kuitembelea Tanzania, itakayofanyika kuanzi tarehe 16-20 Septemba, ambako anatarajia pamoja na kuonana na baadhi viongozi wa Serikali, watafanya mazungumzo na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) yatakayowezesha kusainiwa makubaliano ya ushirikiano kwenye sekta ya nyumba kati ya mashirika hayo mawili.
Aidha, watapata fursa ya kukitembelea kituo cha uwekezaji - TIC ili kupata taarifa muhimu za uwekezaji.
Aidha, Mhe. Mjenga amemuomba Mwenyekiti huyo kufadhili mkutano wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Utalii utakaofanyika Novemba hapa Dubai. Mkutano huo unaandaliwa na Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii ya Tanzania-TTB pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Balozi wa Tanzania Dubai..Mhe. Omar Mjenga akutana na Mwenyekiti wa Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai Description: Rating: 5 Reviewed By: Unknown
Scroll to Top